SERA YETU YA FARAGHA
Sera hii ya faragha huboreshwa mara kwa mara; kila tutakapofanya maboresho, tutatuma katika tovuti yetu na kukutaarifu.
Tumeiboresha sera yetu ya faragha kwa kuwa tuanaboresha na kuanzisha vitu vipya na njia mpya za kufanya kazi.
Hapa tunaeleza namna ya kuchukua, kutumia na kushirikisha taarifa zako binafsi pale unapotumia tovuti hii.
Katika sera hii ya faragha:
HolyStore inaamini na kujikita zaidi katika kulinda faragha ya taarifa binafsi za mtumiaji wa tovuti hii. Tunayapa umuhimu mkubwa masuala ya faragha, usalama na utekelezaji wa sheria za usalama wa taarifa zako.
Tunahakikisha kutekeleza wajibu wetu wa msingi juu ya faragha ya taarifa zako binafsi katika tovuti yetu. Tunalenga kufanya wajibu huu kuwa kipaumbele katika kila jambo tunalofanya.
Mambo ya Msingi
Taarifa binafsi kuhusu wewe tunazochukua
Taarifa tunazochukua kuhusu wewe na namna tunavyozichukua zinaweza kuwa tofauti kulingana na huduma ambazo unatumia au ulizoidhinisha kuzipata, namna ulivyotumia huduma husika, na namna ulivyowasiliana na HolyStore, au kupitia upande wa tatu kwa kibali cha kutushirikisha jambo hilo.
HolyStore itatumia taarifa zako binafsi kwa kuzingatia yafuatayo:
Tutatumia taarifa zako binafsi kwa madhumuni yafuatayo:br>
Kuboresha huduma zetu
Kuboresha na kubuni huduma - Tunachukua taarifa zisizo bainisha majina au taarifa binafsi za jumla ili kuboresha huduma tunazotoa kwa kila mmoja. Hakuna taarifa zozote za uchanganuzi zinazorudi kwako kwa njia yoyote ile.
Kuunda makundi kulingana na sifa (Profiling)
Wakati mwingine tunaweza kuhitaji kukuweka katika kundi fulani kwa ajili ya mambo yanayohusiana na usalama
Tunashughulikia ulinzi madhubuti wa data zako ili kuzilinda na kung’amua viashiria vya matumizi yasiyo sahihi au uharibifu kwa njia yoyote
Namna tunavyoshirikisha wengine taarifa zako binafsi
Pale inapohusika, tunashirikiana taarifa kuhusu wewe na;
Endapo tutafanya mabadiliko ya kimuundo au kuuzwa au kumilikishwa kwa taasisi nyingine tutaipatia hiyo taasisi nyingine taarifa zako
Muunganiko au kuuzwa au kuhamishwa kwa umiliki huu utapendekezwa kufanyika kati yetu na taasisi mojawapo ya kikatoliki kama Baraza la Maaskofu Tanzania
Upande wa tatu tunaofanya nao kazi
Endapo tuna mkataba na mtoa huduma au mzabuni wa kutupatia huduma au kutoa huduma kwa niaba yetu, na wanaweza kupata taarifa zako binafsi, huwa hatuwapi mamlaka ya kuzitumia au kuzitoa isipokuwa tu matumizi hayo yanahusiana na kutoa huduma yao tu
Ukomo wa muda wa kutunza taarifa zako binafsi
Tutatunza taarifa zako kwa muda wote ambao sheria za nchi na sheria za taasisi ya kikatoliki itatutaka. Endapo hakuna matakwa ya kisheria, tutazitunza kwa muda ambao tunahitaji tu
Kuweka salama taarifa zako binafsi
Tuna timu maalum za wataalam wa usalama ambazo kila wakati zinapitia na kuboresha njia za kulinda taarifa zako binafsi dhidi ya kupatikana bila idhini, kupotea kwa bahati mbaya, kuvuja au kuharibika
Hatutakubali kuwajibika endapo taarifa binafsi zitapatikana au kupota bila idhini nje ya uwezo wetu wa kudhibiti
Kamwe hatutakutaka utupe kwa njia zisizo sahihi taarifa zako binafsi au za akaunti ulizoziwekea ulinzi. Unawajibika kutunza taarifa zako binafsi na za akaunti yako na kutozishirikisha kwa watu wengine
Masharti haya yanahusika pia kwa tovuti au mifumo ya upande wa tatu au maudhui unayojiunganisha nayo ili kutumia huduma zetu
Haki ya data binafsi sahihi
Una haki ya taarifa zinazokuhusu kusahihishiwa endapo hazina usahihi. Endapo taarifa zako tulizo nazo zitahitaji kubadlishwa, au unadhani si sahihi, unaweza kutembelea tovuti yetu www.holystore.org au kiunganishi (app) au dawati la huduma ili kubadilisha
Haki ya kupinga matumizi ya data binafsi
Una haki, katika mazingira fulani, kuizuia HolyStore kushughulikia taarifa zako binafsi
Kujitoa katika kupata ujumbe wa shughuli za kanisa na kiroho:
Endapo hutapenda kuendelea kupata ujumbe wa shughuli mbalimbali za kanisa na kiroho, unaweza kuchagua kujitoa katika mawasiliano hayo kupitia tovuti na kwa yale ya muumini kuhusu mambo ya ndani ya parokia yake atapewa maelekezo na uongozi na utaratibu wa parokia husika
Wakati mwingine unaweza kupokea taarifa za parokia nyingine kupitia HolyStore, hata kama wewe si muumini wa parokia hiyo. Hii inaweza kuwa ni mpango wa jimbo husika kueneza taarifa kwa watumiaji wote wa parokia zote zilizopo chini ya jimbo hilo au kwa kutumia parokia mojawapo
Haki ya kudhibiti taarifa zako
Endapo utaona kuwa taarifa zako tulizo nazo si sahihi au unaamini hatutakiwi kuchakata taarifa zako, tafadhali tembelea dawati la Huduma au unaweza kututumia barua pepe kwa info@holystore.org kujadili haki zako. Katika mazingira fulani, utakuwa na haki ya kutuambia tuache kuchakata taarifa zako
Haki ya kufutiwa taarifa
Katika mazingira fulani, kwa mfano, tukiwa hatuna tena sababu ya msingi ya kuendelea kushughulika na taarifa zako au hatuhitajiki na sheria kutunza taarifa hizo, unaweza kuomba tuzifute
Wajibu wa HolyStore Juu ya Faragha
Namna tunavyotunza faragha ya mtumiaji ni sehemu muhimu ya wajibu wetu – iwe ni ulinzi wa taarifa zao binafsi, usiri wa mawasiliano binafsi na namna tunavyoweza kuvuta imani yao kwetu
HolyStore tunalenga kujenga utamaduni ambao watumishi wana ufahamu thabiti juu ya umuhimu wa faragha na namna ya kuhakikisha inalindwa. Wajibu wetu wa Faragha umeweka kanuni zinazoongoza namna tunavyosimamia faragha na namna tunavyowahusisha watumishi wetu na/au wabia (mtu wa tatu) kwenye maswala muhimu - kama vile kulinda faragha au kusaidia kutekeleza sheria za nchi na sheria za taasisi ya kikatoliki
Heshima
Tunathamini faragha kwa sababu ya thamani yake kwa watu. Ni zaidi ya kutekeleza sheria - ni kuhusu kujenga utamaduni unaoheshimu faragha na kuhalalisha imani tuliopewa
Sheria na viwango
Tunazingatia sheria za faragha, na tutafanya kazi na serikali, taasisi za kikatoliki, wadhibiti, watunga sera na watoa maoni kwa ajili ya sheria bora na viwango bora
Uwajibikaji
Tunawajibika kuziishi kanuni hizi kwa familia yetu yote, ikiwa ni pamoja na wabia na watoa huduma wetu

-
“sisi” inamaanisha HolyStore;
-
“wewe” inamaanisha Parokia/Jimbo au taasisi yoyote ya kikatoliki inayotumia mfumo huu au mtumiaji mmojammoja muumini wa kanisa katoliki.
-
“upande wa tatu” inamaanisha mtu ambaye si wewe au sisi; watoa huduma za ziada kama mitandao ya simu au benki au intaneti au mamlaka za usimamizi chini ya sheria za Jumhuri ya Muungano wa Tanzania
-
Tumesajiliwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya namba ya kampuni 477394
HolyStore inaamini na kujikita zaidi katika kulinda faragha ya taarifa binafsi za mtumiaji wa tovuti hii. Tunayapa umuhimu mkubwa masuala ya faragha, usalama na utekelezaji wa sheria za usalama wa taarifa zako.
Tunahakikisha kutekeleza wajibu wetu wa msingi juu ya faragha ya taarifa zako binafsi katika tovuti yetu. Tunalenga kufanya wajibu huu kuwa kipaumbele katika kila jambo tunalofanya.
Mambo ya Msingi
Taarifa binafsi kuhusu wewe tunazochukua
Taarifa tunazochukua kuhusu wewe na namna tunavyozichukua zinaweza kuwa tofauti kulingana na huduma ambazo unatumia au ulizoidhinisha kuzipata, namna ulivyotumia huduma husika, na namna ulivyowasiliana na HolyStore, au kupitia upande wa tatu kwa kibali cha kutushirikisha jambo hilo.
HolyStore itatumia taarifa zako binafsi kwa kuzingatia yafuatayo:
- Utekelezaji wa mkataba wako au kuingia mkataba na kuchukua hatua kulingana na maombi yako. Kwa mfano, ili uweze kuungalishwa na huduma inayohita upande wa tatu mfano huduma ya ujumbe mfupi kwa simu za mkononi, huduma ya malipo kwa mitandao ya simu au huduma za uunganishwa wa akaunti ya benki kuwezeshwa kupokea miamala kutoka mitandao ya simu
- Maslahi halali ya kuboresha na kutoa huduma za mfumo na tovuti ya HolyStore, kwa mfano, kuzuia udanganyifu, kuimarisha usalama wa mfumo na huduma na uboreshaji wa huduma zetu. Kila tunapozingatia msingi huu halali kuchakata data zako, tunatathmini maslahi yetu ya kukuhudumia kuhakikisha kuwa hayazidi haki zako
- Utekelezaji wa matakwa ya lazima ya sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au sheria ya taasisi ya kanisa katoliki, ambayo yako chini ya sera madhubuti za ndani, taratibu, na haki yako ya kuweka mipaka ya matumizi ya data, ambayo inadhibiti wigo wa msaada kulingana na sheria itakayotakiwa kutolewa
- Ridhaa unayotoa pale ambapo HolyStore haijiegemezi kwenye msingi wowote wa kisheria. Ridhaa hiyo inaweza kuondolewa muda wowote
- Unapokuwa umetoa idhini kwa upande wa tatu, kama vile wabia wetu wa huduma au wazabuni wa upande wa tatu, kupata taarifa zinazokuhusu
- Unapojisajili kwaajili ya kutumia huduma mahsusi
- Unapojiunga na vijarida, taarifa na huduma zingine kutoka kwetu
- Unapowasiliana nasi kupitia njia mbalimbali, au unapoulizia taarifa kuhusu huduma
- Unapotembelea au unapovinjari tovuti yetu
- Pale taarifa zako zinapokuwa wazi kupatikana
- Jina lako, anuani, namba ya simu, tarehe yako ya kuzaliwa, jinsia na anuani ya barua pepe
- Taarifa zako za kibenki kwa parokia inayounganishwa kupokea malipo kwa njia ya mitanda ya simu za mkononi
- Mawasiliano yako na sisi, kama ujumbe au simu, maongezi ya ana kwa ana, barua pepe au barua uliyotutumia au kumbukumbu yoyote ya mawasiliano yako na sisi
- Taarifa za uthibitisho – tutachukua namba ya siri (nywila), viashiria na taarifa za kiusalama kama hizo zinazotumika kwa ajili ya uthibitisho na kuingia kwenye akaunti au kupata huduma
- Kiwango cha huduma unayopata – kwa mfano matatizo ya mtandao au huduma na matukio mengine yanayoweza kuathiri huduma zetu huduma zingine za kiroho kwa taasisi ya kikatoliki
- Taarifa za matumizi ya huduma maalum, kama - Kila unapotumia simu yako ya kiganjani kufanya malipo ya zaka au sadaka nyingine katika parokia yako, kumbukumbu huwekwa. Hii inajumuisha namba yako ya simu, aina ya mtandao unaotumia, namba ya muamala husika, tarehe na muda huduma ilipofanyika au kutuma ujumbe (SMS)
Tutatumia taarifa zako binafsi kwa madhumuni yafuatayo:br>
- Kushughulikia huduma unayohitaji kutoka wetu, na kukuhabarisha kuhusu hatua tuliyofikia katika kushughulikia ombi lako
- Kukupa bili ya kutumia huduma zetu, au huduma sahihi kutoka kwa wabia wa upande wa tatu kama huduma za mitandao ya simu kama ujumbe (SMS), kamisheni za malipo kutumia mitandao ya simu
- Kuwasiliana nawe endapo taarifa za kutoa bili ulizotupa zinakaribia kuisha muda wake au tunashindwa kufanya malipo
- Kujibu maswali yoyote au dukuduku unazoweza kuwa nazo kuhusu huduma zetu
- Tutawasiliana nawe kwa ujumbe wa dawati la huduma ili kukuhabarisha taarifa mpya kuhusu huduma mpya. Kwa mfano, mabadiliko ya vigezo na masharti, mpango wa bei na matumizi ya data, maboresho unayoweza kuwa unastahili na huduma za kukuwezesha kutumia mtandao unapohama mipaka ya nchi au kukatika kwa huduma kutoka na sababu kadhaa
- Kushughulikia matatizo ya kiufundi endapo utakutana nayo
Kuboresha huduma zetu
Kuboresha na kubuni huduma - Tunachukua taarifa zisizo bainisha majina au taarifa binafsi za jumla ili kuboresha huduma tunazotoa kwa kila mmoja. Hakuna taarifa zozote za uchanganuzi zinazorudi kwako kwa njia yoyote ile.
Kuunda makundi kulingana na sifa (Profiling)
Wakati mwingine tunaweza kuhitaji kukuweka katika kundi fulani kwa ajili ya mambo yanayohusiana na usalama
Tunashughulikia ulinzi madhubuti wa data zako ili kuzilinda na kung’amua viashiria vya matumizi yasiyo sahihi au uharibifu kwa njia yoyote
Namna tunavyoshirikisha wengine taarifa zako binafsi
Pale inapohusika, tunashirikiana taarifa kuhusu wewe na;
- Taasisi na mamlaka za kikatoliki za kusimamia, kuratibu, kuasisi taarifa za wakatoliki kwa shughuli ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
- Taasisi na mamlaka za kikatoliki za kutunga na kusimamia sheria za kikatoliki ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
- Upande wa tatu (Makampuni) unaohusika kutoa huduma kwa ajili ya, au kwa niaba ya, HolyStore mfano makampuni ya simu kwa ajili ya huduma za simu, ujumbe mfupi (SMS) au mabenki kwa taarifa za kifedha
- Upande wa tatu kwa ajili ya maboresho ya huduma na usalama wa data
- Upande mwingine wa tatu pale unapoingia mkataba wa kutumia huduma zao na wakahitaji taarifa zako kwa ajili ya uthibitisho na kuzuia udanganyifu
- Upande wa tatu ambao tunatangaza nao biashara zetu, kama vile,
- Tutatoa taarifa zako endapo itafaa kwa madhumuni ya kujilinda dhidi ya udanganyifu, kulinda haki au mali zetu, au kulinda maslahi taasisi ya kikatoliki.
- Tunaweza pia kutoa taarifa zako ili kutekeleza wajibu wetu wa kisheria wa kutekeleza matakwa ya kisheria ya mamlaka. Taarifa zako binafsi zitatolewa pale ambapo tu sisi katika nia njema tunawajibika kisheria kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria za nchi na sheria za taasisi ya kikatoliki na baada ya kufanya tathmini ya kina ya matakwa yote ya kisheria